Monday, 25 September 2017
RAIS MAGUFULI ATANGAZA NAFASI ZA AJIRA 3,000 ZA WANAJESHI WALIOPITIA JKT KIPAUMBELE
JPM ATANGAZA AJIRA 3,000 ZA JESHI, AJUTA KUWA RAIS
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametangaza ajira mpya 3,000 za jeshi ili kuongeza nguvu kazi katika jeshi la wananchi wa Tanzania.
Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo wakati akihutubia wakazi wa Arusha waliohudhuiria kushuhudia zoezi la kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa JWTZ 422 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Miongoni mwa mambo aliyozungumza katika hotuba yake, Rais Magufuli amesema anajuta kuwa rais kutokana dosari nyingi alizozikuta karibu kila sehemu ikiwemo ufisadi na wafanyakazi hewa.
Amesema “Nimeamua kuwa sadaka kwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi... naamini hapatatokea mwingine atakayejitoa hivi”
Kuhusu Kuhamia Dodoma, amesema mwaka huu makamu wa rais atahamia Dodoma na mwakani yeye mwenyewe atahamia huko huku akionya watakaobaki Dar es Salaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Manchester United yaingiwa na hofu juu ya Jose Mourinho
Ripoti kutoka nchini Uingereza hii jana zinasema klabu ya Manchester United imenza kuwa na hofu juu ya kocha Jose Mourinho kwani anahisiwa ...

-
Ripoti kutoka nchini Uingereza hii jana zinasema klabu ya Manchester United imenza kuwa na hofu juu ya kocha Jose Mourinho kwani anahisiwa ...
-
BREAKING NEWS: Matokeo Ya Darasa la Saba 2017 Yametoka HAYA HAPA MATOKEO DARASA LA SABA 2017 KUONA MATOKEO BONYEZA HAPO>>>...
No comments:
Post a Comment