Tuesday, 31 October 2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WAOMBAJI WA KADA YA AFYA

OR TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika. 
Aidha, mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. 
Kuona Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi >>>>> BONYEZA HAPA 

Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo, watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika. 

Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya zitatangazwa mara baada ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa vyeti. Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi. 

Limetolewa na:- 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 
OR – TAMISEMI
30/10/2017

No comments:

Post a Comment

Manchester United yaingiwa na hofu juu ya Jose Mourinho

Ripoti kutoka nchini Uingereza hii jana zinasema klabu ya Manchester United imenza kuwa na hofu juu ya kocha Jose Mourinho kwani anahisiwa ...