Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyengine amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya kumchagua rais mpya siku ya Alhamisi.
Rais Uhuru ambaye alikuwa akiwahutubia Wakenya amesema kuwa kila mkenya ana haki ya kushiriki ama kutoshiriki katika uchaguzi huo na kwamba serikali yake itawapatia usalama Wakenya wote.
Amesema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa kama taifa la kidemokrasia na kwamba taifa hilo litaimarika zaidi baada ya uchaguzi wa alhamisi.
Hatahivyo amewaonya wale walio na mpango wa kuvuruga uchaguzi huo kwamba serikali haitawaruhusu.
''Tafadhalini baada ya kushiriki katika shughuli ya upigaji kura nenda nyumbani kwa jirani yako muendelee kuishi kama mulivyokuwa mukiishi kwa kuwa yeye ndio ndugu yako na dadaako, uchaguzi huu haufai kuwagawanya maana kuna siku za kuishi baadaye'', alisema Uhuru Kenyatta.
Amesema kuwa ni sharti Wakenya kufuata katiba waliopitisha 2010 ambayo inawapatia fursa mpya ya kumchagua rais wao kwa kipindi chengine cha miaka mitano.
Amesema kuwa vyombo vyote vya usalama vimesambazwa Kenya nzima ili kuwalinda Wakenya.
Odinga amesema upinzani sasa umegeuza muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) kuwa kundi la pingamizi dhidi ya serikali, kundi la kupinga serikali.
"Utakuwa ni muungano wa ukombozi," amesema.
"Tumesema hatutaheshimu serikali dhalimu."
Wamesema wataanza kususia mambo muhimu kwenye serikali, watasusia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni zinazounga mkono utawala na wataendelea kushinikiza uchaguzi utafanyika katika siku 90.
"Uchaguzi wa kesho ni uchaguzi wa Jubilee. Ni shughuli tu ya maonesho. Ni Uhuru akishindana na Kenyatta. Na wanasema Uhuru na Kenyatta wamekaribiana sana, na hata wanakaribia kwenda duru ya pili," amesema.
No comments:
Post a Comment