Tuesday, 31 October 2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI KWA WAOMBAJI WA KADA YA AFYA

OR TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika. 
Aidha, mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. 
Kuona Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi >>>>> BONYEZA HAPA 

Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo, watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika. 

Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya zitatangazwa mara baada ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa vyeti. Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi. 

Limetolewa na:- 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 
OR – TAMISEMI
30/10/2017

Wednesday, 25 October 2017

Nafasi za kazi NIMR zatangazwa

On behalf of the National Institute for Medical Research (NIMR), Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) and Tanzania Bureau of Standards (TBS), President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 28 vacant posts as mentioned below;
To see VACANCIES ANNOUNCED>>>> CLICK HERE

Uhuru Kenyatta awataka Wakenya kushiriki uchaguzi wa marudio

Uhuru Kenyatta awataka Wakenya kushiriki uchaguzi
Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyengine amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya kumchagua rais mpya siku ya Alhamisi.
Rais Uhuru ambaye alikuwa akiwahutubia Wakenya amesema kuwa kila mkenya ana haki ya kushiriki ama kutoshiriki katika uchaguzi huo na kwamba serikali yake itawapatia usalama Wakenya wote.
Amesema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa kama taifa la kidemokrasia na kwamba taifa hilo litaimarika zaidi baada ya uchaguzi wa alhamisi.
Hatahivyo amewaonya wale walio na mpango wa kuvuruga uchaguzi huo kwamba serikali haitawaruhusu.
''Tafadhalini baada ya kushiriki katika shughuli ya upigaji kura nenda nyumbani kwa jirani yako muendelee kuishi kama mulivyokuwa mukiishi kwa kuwa yeye ndio ndugu yako na dadaako, uchaguzi huu haufai kuwagawanya maana kuna siku za kuishi baadaye'', alisema Uhuru Kenyatta.
Amesema kuwa ni sharti Wakenya kufuata katiba waliopitisha 2010 ambayo inawapatia fursa mpya ya kumchagua rais wao kwa kipindi chengine cha miaka mitano.
Amesema kuwa vyombo vyote vya usalama vimesambazwa Kenya nzima ili kuwalinda Wakenya.
Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Odinga: Tumegeuza Nasa kuwa vuguvugu la pingamizi dhidi ya serikali

Odinga amesema upinzani sasa umegeuza muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) kuwa kundi la pingamizi dhidi ya serikali, kundi la kupinga serikali.
"Utakuwa ni muungano wa ukombozi," amesema.
"Tumesema hatutaheshimu serikali dhalimu."
Wamesema wataanza kususia mambo muhimu kwenye serikali, watasusia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni zinazounga mkono utawala na wataendelea kushinikiza uchaguzi utafanyika katika siku 90.
"Uchaguzi wa kesho ni uchaguzi wa Jubilee. Ni shughuli tu ya maonesho. Ni Uhuru akishindana na Kenyatta. Na wanasema Uhuru na Kenyatta wamekaribiana sana, na hata wanakaribia kwenda duru ya pili," amesema.

Friday, 20 October 2017

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KCMC


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) anapenda kuwataarifu Waombaji kazi wote walioomba kazi za KCMC kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26 - 27 Oktoba, 2017 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi Waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) anapenda kuwataarifu Waombaji kazi wote walioomba kazi za KCMC kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26 - 27 Oktoba, 2017 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi Waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. 

KUONA MAJINA YA WALIWOITWA KWENYE KWENYE USAILI.>>>> BONYEZA HAPA

MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA DARASA LA SABA (PSLE) 2017 YAMETANGAZWA.

BREAKING NEWS: Matokeo Ya Darasa la Saba 2017 Yametoka



HAYA HAPA MATOKEO DARASA LA SABA 2017

KUONA MATOKEO BONYEZA HAPO>>>>>http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

Manchester United yaingiwa na hofu juu ya Jose Mourinho

Ripoti kutoka nchini Uingereza hii jana zinasema klabu ya Manchester United imenza kuwa na hofu juu ya kocha Jose Mourinho kwani anahisiwa ...