Thursday, 9 November 2017

OBREY CHIRWA ANG'ARA ZAIDI YA IBRAHIM AJIBU NA ERASTONYONI

Image result for CHIRWA

Mshambuliaji wa Young Africans , Obrey Chirwa amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa Oktoba wa Ligi Kuu ya ya Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/2018.

Mshambuliaji huyo amedaiwa kutoa mchango mkubwa kwa klabu yake ya Young Africans mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.

Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. bao la Yanga lilifungwa
na Chirwa.

Chirwa raia wa Zambia alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajib pia wa Yanga alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

No comments:

Post a Comment

Manchester United yaingiwa na hofu juu ya Jose Mourinho

Ripoti kutoka nchini Uingereza hii jana zinasema klabu ya Manchester United imenza kuwa na hofu juu ya kocha Jose Mourinho kwani anahisiwa ...