Wasailiwa waliochaguliwa (Selected) wanatakiwa kufika katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira-Maktaba Kuu ya Taifa, kwa ajili ya usaili wa Mahojiano (Oral) siku ya tarehe 07/11/2017 saa moja kamili asubuhi, wakiwa na vyeti vyao halisi (Original Certificates)
Kuona waliochaguliwa >>>>> BOFYA HAPA
Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyengine amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya kumchagua rais mpya siku ya Alhamisi.
Rais Uhuru ambaye alikuwa akiwahutubia Wakenya amesema kuwa kila mkenya ana haki ya kushiriki ama kutoshiriki katika uchaguzi huo na kwamba serikali yake itawapatia usalama Wakenya wote.
Amesema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa kama taifa la kidemokrasia na kwamba taifa hilo litaimarika zaidi baada ya uchaguzi wa alhamisi.
Hatahivyo amewaonya wale walio na mpango wa kuvuruga uchaguzi huo kwamba serikali haitawaruhusu.
''Tafadhalini baada ya kushiriki katika shughuli ya upigaji kura nenda nyumbani kwa jirani yako muendelee kuishi kama mulivyokuwa mukiishi kwa kuwa yeye ndio ndugu yako na dadaako, uchaguzi huu haufai kuwagawanya maana kuna siku za kuishi baadaye'', alisema Uhuru Kenyatta.
Amesema kuwa ni sharti Wakenya kufuata katiba waliopitisha 2010 ambayo inawapatia fursa mpya ya kumchagua rais wao kwa kipindi chengine cha miaka mitano.
Amesema kuwa vyombo vyote vya usalama vimesambazwa Kenya nzima ili kuwalinda Wakenya.

